Mambo ya Kufanya Mara Baada ya Kupoteza (Ibiwa) Simu

Fanya haya mara baada ya kupoteza simu yako!

Mambo ya Kufanya Mara Baada ya Kupoteza Simu

Mambo ya Kufanya Mara Baada ya Kupoteza (Ibiwa) Simu

Mambo guys! Girlfriend wangu aliibiwa simu akipanda gari la abiria (daladala) hivi karibuni pindi atokapo kazini, muda wa saa moja jioni, Machi 13, 2023. Alidhoofu sana, hata hakujua nini afanye kwa muda ule!

Hudhuni ilimtawala. Nadhani hivi ndivo kila mmoja huwa pindi apotezapo kitu yeye hukihusudu. Simu aliyoibiwa ili kuwa janja yani smartphone, hivyo, alianza tumia simu yake ndogo (kitochi) ambayo alikuwa akitumia kama back up.

Si wengi walikuwa wakiifaham namba ya simu yake hiyo ya pembeni. Alimpigia mama yake ili kumjulisha upotevu wa simu yake, na kwakuwa hakuwa na namba nyingi zimehifadhiwa kwa simu hiyo, basi alimuomba mama yake aendelee kuwajulisha na wengine ili wasiwe na wasiwasi naye.

Alfajiri ilipofika, mimi nilipokea simu kadhaa, watu wakiulizia yuko wapi (kwa sababu alichelewa kufika kazini) na nini kinaendelea kwake?

Nilistaajabu kwa sababu haikuwa kawaida mimi kupigiwa simu na kuulizwa vile!

Related: Watanzania, kwani Magufuli Aliwezaje?

Ghafla, nilipokea simu ya mfanyakazi mwenzake (yeye ninamfahamu) akiuliza wapi girlfriend wangu alipo na akanieleza yakuwa amepokea ujumbe mfupi (SMS) ikimuomba pesa ya kuwa yuko na matatizo ayasovu.

Sikushangaa kwa sababu nilikuwa naelewa nini kilitokea jana (yeye kuibiwa simu), kilichonistusha ni kuhusu sms zinazotumwa!

Nilimjibu…

Puuzia jumbe hizo, kwani amepoteza simu jana, nadhani ni wao wezi wanajaribu kutapeli kwa jinsi hiyo…

Nilimpigia girlfriend wangu kwa simu yake ya back up na kumueleza kuhusu simu zote nilizopokea na kumuomba aende kwenye maduka ya mitindao yote aliyokuwa akitumia ili waweza zuia huduma kwenye namba hizo mpaka siku atakapo taka renew laini hizo.

Alikwenda na kufanya kama tulivo kubalianaa.

Huduma zilizuia papo hapo, lakini tayari alikuwa keshachelewa, punde alipokea simu kutoka kwa mama yake akiambiwa yakuwa tayari rafiki yake Queen alikuwa keshaingia kingi na kutuma pesa kiasi cha milioni mbili kwa matapeli hao.

Masaa machache tu yalitosha kufanya udanganyifu mkubwa ambao ulimtia hasara mdada huyo na kumpa mawazo Dorice ambaye ndiye girlfriend wangu.

Alienda police na kutoa taarifa, aliandikiwa RB na kukabidhiwa kwa afande atakaeisimamia kesi yake ya ufuatiliaji wa wapi ilipo yake simu iliyoibiwa (tracking).

Mambo ya Kufanya Mara Baada ya Kupoteza Simu RB
RB iyoandikwa na polisi, Dodoma.

Nilifika kituoni hapo, kesi ilifunguliwa na hapo afande in-charge wa kesi alitueleza mambo ya kufanya haraka baada ya kupotelewa (ibiwa) na simu…

Mambo mawili ya kufanya punde tu uibiwapo/upotelewapo na simu..

1. Ripoti haraka upotevu wa simu kwa mtandao husika uutumiawo

Tulishauliwa kutoa taarifa haraka kuhusu upotevu wa simu ili ziwezwe kuzuiliwa huduma, hii husaidia kuepusha matumizi mabaya ya laini yako.

Nini faida ya kufanya hivi?

Ukiripoti, laini hupoozeshwa, na hata laini ikitolewa kutoka kwenye simu hiyo kwenda simu nyingine, contacts hazitoweza onekana hata kwa mbinu yoyote. Kwa kingereza wanasema hidden.

Hivyo, kama angelifanya hivyo mapema, wezi hawo wasingeweza pata namba hizo kwa kuwa simu ilikuwa na lock (nywila), na hata kawa wangeli hamisha laini kwenda kwenye simu nyingine, contacts zisingeonekana.

2. Ripoti upotevu wa simu yako kituo chochote cha polisi kilicho karibu nawe

Baada ya kufanya kama tulivyoona namba moja, sasa unaweza kwenda kuripoti kuhusu upoteveu wa simu yako kituo chochote cha polisi kilicho karibbu nawe.

Utaulizwa maswali machache yatakayoisaidia upatikanaji wa simu yako. Na bila kusahau, utaelekezwa nini ufanye haraka ili laini yako isitumike vibaya baada ya kupotea.

Nini sisi tulifanya ili tupate simu iliyopotea na pesa zilizotapeliwa?

Afande tuliokabidhiwa alikuwa akijihusisha na masuala ya Cyber, hivyo alikuwa akijua (wewe pia unaweza kuwa ushajua) nini anatakiwa kufanya.

Huu ni mfumo wa kutrack simu (kiteknolojia) na kufaham wapi ilipo. Tuliambiwa tusubiri siku kadhaa hadi kifaa hiko kitambua lokesheni halisi wapi simu ipo.

Hatukuishia hapo, tulikodisha mjuzi wa mambo hayo (Cybersecurity Specialist) private ili atufanyie kazi yetu kama si tupendavyo. Si unajua tena huwezi pangia wafanyakazi wa kiserikali kama wewe si mkuu wa kazi yao!

Yeye pia alituambia tusubiri wiki mbili ili tupate ripoti sahihi, hatukuwa na budi bali kusubiri, leo ni siku ya nne, tutawajuza kama tulifanikiwa au la hivi karibuni, usikose kuja kuangalia update ijayo.

Na tafadhari usisahau kushare na wenzio ili wajue nini wanatakiwa kufanya mara baada wapotezapo simu zao.

Kuweni makini, msisahau kutunza vifaa hivyo!

 

Do you find Offblogmedia useful? Click here to give us five stars rating!

 
About KelvinDerola 3541 Articles
Kelvin Dérola is a certified Journalist who has received his degree in Journalism from St. Augustine University. From May 21st 2022 to the present day, he is running this awesome website. When he isn't blogging, he is playing GTA or COD with friends or just listening to some new music. Wanna talk? Phone: +255 716 805 652 Email: [email protected]

Join the Discussion

No one has commented yet. Be the first!

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*